Man U waweka Dau kwa Club inayomtaka Maguire

Manchester United wameweka thamani inayotakiwa ya £50m kwa klabu inayotaka kumnunua beki wa England Harry Maguire, 30. (Manchester Evening News)

West Ham wanatumai kumnunua kiungo wa kati wa England James Ward-Prowse, 28, kwa ada ya £20m lakini Southampton wanataka karibu £40m kwa ajili ya nahodha wao huyo (Mail)

Wolves wanakaribia kumsajili tena beki wa pembeni wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 31, baada ya kuondoka Atletico Madrid. (TeamTalk)

Uhamisho wa kipa wa Cameroon Andre Onana wa pauni milioni 43 kutoka Inter Milan kwenda Manchester United uko katika hatua za mwisho na utakamilika wiki hii baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kukubaliana maslahi binafsi.

Source: BBC

UP