Posted on Leave a comment

Kim Kardashian atokewa na Mzimu

Mwanamitindo, X na babe mama wa Kanye West, Kim Kardashian ameshtushwa na Kivuli kinachomuonesha Mwanamke mwingine kwenye picha ambayo Kaipiga kama Selfie akiwa mwenyewe.

Kwenye Picha hii ambayo ameipost kwenye Instagram Kim anasema ameshangaa baada ya kuiangalia picha aliyoichukua mwenyewe “Selfie” akiwa mwenyewe kuonekana kivuli cha mwanamke anayehisi ni Mzimu kwani wakati anajipiga picha hiyo alikuwa mwenyewe ila ameshangaa kuona kivuli cha mwanamke nyuma yake.

Kwenye Caption ameandika:- Soooo I took this pic last week when I was alone and now going through my phone I am freaking out noticing a woman in the window

Posted on Leave a comment

Tanasha arudi alipoanzia

Kama ni mtu unayefuatilia, Industry ya Burudani ilianza kumjua Staa wa Kenya Tanasha Donna kupitia Uigizaji wa kwenye Video za Muziki (Video Vixen)

Video ya kwanza ambayo Alionekana ilikuwa Nagharamia, Wimbo wa Ali Kiba na Christian Bella iliyotoka Miaka 7 Iliyopita.

Baadae akawa Mtangazaji wa Kituo cha Radio ya NRG Nchini Kenya ambapo huko ndiko alikokutana na Baba Mtoto wake “Diamond Platnumz”

Kilichofuata baada ya ustaa kumwagiwa Petrol na Mond, Tanasha akajitupa kwenye Muziki ambapo mpaka Sasa ni mmoja kati ya Wasanii wenye Majina Kenya.

Lakini Pamoja na ukubwa huo, bado Tanasha ukienda na Offer inayoeleweka au akikuelewa Bado yupo tayari kuwa Video Vixen kwenye Video yako na ndiyo maana amehusika kama Video Vixen kwenye Video Mpya ya Msanii wa Nigeria Lojay inayokwenda kwa jina la OVA iliyotoka siku 4 zilizopita

CHUNGULIA CHUPA HILO HAPA CHINI KISHA TUPE COMMENT YAKO