Tamasha la kila mwaka la Africa Music Now linaloandaliwa na Msanii Mkongwe wa Hip-Hop Kutoka Arusha, Chindo Man, linafanyika tena mwaka huu.
Tamasha hilo lenye Dhamira Kuu ya kuonyesha na Kukuza Vipaji Jijini Arusha na Tanzania kiujumla linafanyika Jumamosi hii Tarehe 29/7/2023 katika Kiwanja maarufu Arusha, Billy’s River.
Pamoja na Chindo Man Mwenyewe, Wasanii wengine Watakaotumbuiza mwaka huu ni Pamoja na @dipper_rato @djdavizotz @jcbwatengwa @machaliiwatundu @warriorsfromtheeast @mopluschanya @marleen_xplastaz @pindabway na @maasaiblonde huku Host akiwa @mrslema
Viingilio ni Shilingi Buku 5 kwa Kawaida na Sh. Buku 10 kwa V.I.P
Usikose Tamasha hili.
