Maisha ya Davido yako Hatarini, aaswa kuikimbia Nigeria !!!

Kutokana na Sakata linaloendelea Kumuhusu Staa wa Muziki Nigeria, David Adeleke maarufu kama Davido baada ya Video ya video ya Msanii wake kutafsiriwa kama Kuidhalilisha Dini ya Kiislam, Staa huyo ameaswa kuikimbia Nigeria yeye na Msanii wake kwani maisha yake yako Hatarini kutokana na Hasira za Waislam Nigeria.

Balaa hilo limemuandama Davido baada ya kupost Trailer ya Wimbo wa Msanii wake aliyemsaini aitwaye Logos Olori.

Kwenye kipande alichopost Davido cha wimbo uitwao ‘Jaye Lo’ wanaonekana Watu wakiwa Nje ya Msikiti na Mavazi ya Kiislam na baada ya kumaliza Kusali wanaonekana Wanacheza Mziki, Video ambayo Imetafsiriwa kama Davido na Msanii wake Wameidhalilisha Dini ya Kiislam kiasi kwamba Waislam wengi Duniani wamemtaka Davido kuomba Radhi lakini Mpaka sasa ni siku nne zimepita Davido hajafanya hivyo.

Tumeshuhudia Akichimbwa Mikwara kutoka sehemu mbali mbali Duniani huku kwao Nigeria Tumechungulia Mabango yenye Picha zake Yakiharibiwa na Waislam wenye Hasira Kali.

Kufuatia sakata hilo, Mwandishi wa Habari Maarufu kutoka Nigeria Kemi Olunloyo amemuasa Davido kuikimbia Nigeria yeye na Msanii wake kwani Usalama wake ni Mdogo kwa hiki kinachoendele.

Kemi Olunloyo

Mwanahabari huyo ameandika:-

Davido leave Nigeria with your artist. Get him a visa ASAP. You are in danger in Nigeria. Big Danger. Apologize to Islam. I have credible information that these credible threats are realm I was very quiet during the Deborah case.

I was dealing with the Oromoni threats which I now posted after 2 years. I was reading what this girl was writing on WhatsApp and vowed never to apologize. LEAVE!! LEAVE!! LEAVE!! Ignore your dáft fans saying it’s not your video.

You wrote the concept. You paid $70k, even the video director needs protection. They are not even “begging on your behalf, the Nigerian way”. If these people harm you, these fans will be the first to post”

UP