Posted on Leave a comment

Bruce Africa – Jojina (Official Music Video)

Baada ya kufanya poa na Ngoma yake iliyokuwa Hit ya Africa inayokwenda kwa Jina la YOU ambayo Video yake kwa sasa ina Views almost 4M, ngoma iliyofuatiwa na mkwaju mwingine uitwao MY LOVE, Staa wa Muziki kutoka Arusha, BRUCE AFRICA a.k.a Boyfriend ameachia Hit nyingine kwa jina JOJINA

Bruce Africa
Bruce Africa

Kwenye Jojina, Bruce anaelezea namna ambavyo amedata kwa Binti Jojina ambaye anakiri walishafanya mpaka Tambiko.

HII HAPA VIDEO YA JOJINA

KAMA ULIMISS YOU NA MY LOVE HIZI HAPA CHINI:-

Posted on Leave a comment

Kizz Daniel Kuidondosha “MAVERICK”

Kufuatia mafanikio makubwa ya nyimbo zake kama BUGA, COUGH, RTID & SHUPERU, Kizz Daniel ametangaza jina la albamu mpya “MAVERICK”.

Mkali wa Afrobeats, Kizz Daniel, anatazamiwa kuwapeleka mashabiki wake katika safari ya kufurahisha na albamu yake inayokuja, “Maverick.” Msanii huyo anayetambulika kimataifa, Mr. Vado The Great, amekuwa akivuka mipaka ya ubunifu katika muziki wake, na kwenye “Maverick” anaahidi kuwa Album yake Mpya hii itamuelezea yeye ni nani.

Ameweka wazi kwamba Album yake hiyo ataiachia rasmi ijumaa tarehe 28/7/2023

Katika albamu hii, Kizz Daniel anaweka wazi nafsi yake, akitoa kipande chake ambacho amekificha kwa muda.

Nikimnukuu “The only thing that kept coming to my mind when we were making this album was pretty much, I want to do what I know how to do, I want to make music the way I want to make music. For Maverick, It’s my expression, I think the inspiration about it just explained itself now. I want to give a piece of me that I have been hiding all this while.”

HII HAPA NI TRAILER YA ALBUM HIYO

NA HAYA HAPA CHINI NI MAJINA YA NGOMA ZITAKAZOPATIKANA KWENYE ALBUM HIYO:

 1. RED & GREEN
 2. MY G
 3. FLEX
 4. COUGH
 5. SHOW YOU OFF
 6. SHUPERU
 7. BUGA
 8. FERAN YOU TWO
 9. FERAN MI
 10. COMPLICATED
 11. E’BETTER
 12. BLOOD IS THICKER
 13. ONE DOLLAR
 14. EASY TO LOVE
 15. POUR
 16. NEVER
 17. ANCHOVY
 18. RITD
 19. SIDE CHICK
 20. COUGH REMIX.

Posted on Leave a comment

Africa Music Now Festival Kuitikisa – Arusha

Tamasha la kila mwaka la Africa Music Now linaloandaliwa na Msanii Mkongwe wa Hip-Hop Kutoka Arusha, Chindo Man, linafanyika tena mwaka huu.

Tamasha hilo lenye Dhamira Kuu ya kuonyesha na Kukuza Vipaji Jijini Arusha na Tanzania kiujumla linafanyika Jumamosi hii Tarehe 29/7/2023 katika Kiwanja maarufu Arusha, Billy’s River.

Pamoja na Chindo Man Mwenyewe, Wasanii wengine Watakaotumbuiza mwaka huu ni Pamoja na @dipper_rato @djdavizotz @jcbwatengwa @machaliiwatundu @warriorsfromtheeast @mopluschanya @marleen_xplastaz @pindabway na @maasaiblonde huku Host akiwa @mrslema

Viingilio ni Shilingi Buku 5 kwa Kawaida na Sh. Buku 10 kwa V.I.P

Usikose Tamasha hili.

Posted on Leave a comment

Travis Scott Kuidondosha “Utopia”

Albamu ya “Utopia” iliyosubiriwa kwa muda mrefu ya Travis Scott inaonekana kuwasili hivi karibuni huku tukio la uzinduzi wa albamu ya Utopia likitarajiwa kufanyika Cairo, Misri, kwenye Pyramids of Giza.

Utopia itakuwa na kazi 5 binafsi za sanaa, vinyls, CD na maagizo ya mapema[set pre-orders].

Zaidi ya hayo, Travis pia ataperform  albamu yake pia.

Travis amekuwa akifanya kazi kwenye album yake ya Utopia tangu 2020, lakini tarehe rasmi ya kutolewa iliendelea kusogezwa mbele.