Posted on Leave a comment

Maisha ya Davido yako Hatarini, aaswa kuikimbia Nigeria !!!

Kutokana na Sakata linaloendelea Kumuhusu Staa wa Muziki Nigeria, David Adeleke maarufu kama Davido baada ya Video ya video ya Msanii wake kutafsiriwa kama Kuidhalilisha Dini ya Kiislam, Staa huyo ameaswa kuikimbia Nigeria yeye na Msanii wake kwani maisha yake yako Hatarini kutokana na Hasira za Waislam Nigeria.

Balaa hilo limemuandama Davido baada ya kupost Trailer ya Wimbo wa Msanii wake aliyemsaini aitwaye Logos Olori.

Kwenye kipande alichopost Davido cha wimbo uitwao ‘Jaye Lo’ wanaonekana Watu wakiwa Nje ya Msikiti na Mavazi ya Kiislam na baada ya kumaliza Kusali wanaonekana Wanacheza Mziki, Video ambayo Imetafsiriwa kama Davido na Msanii wake Wameidhalilisha Dini ya Kiislam kiasi kwamba Waislam wengi Duniani wamemtaka Davido kuomba Radhi lakini Mpaka sasa ni siku nne zimepita Davido hajafanya hivyo.

Tumeshuhudia Akichimbwa Mikwara kutoka sehemu mbali mbali Duniani huku kwao Nigeria Tumechungulia Mabango yenye Picha zake Yakiharibiwa na Waislam wenye Hasira Kali.

Kufuatia sakata hilo, Mwandishi wa Habari Maarufu kutoka Nigeria Kemi Olunloyo amemuasa Davido kuikimbia Nigeria yeye na Msanii wake kwani Usalama wake ni Mdogo kwa hiki kinachoendele.

Kemi Olunloyo

Mwanahabari huyo ameandika:-

Davido leave Nigeria with your artist. Get him a visa ASAP. You are in danger in Nigeria. Big Danger. Apologize to Islam. I have credible information that these credible threats are realm I was very quiet during the Deborah case.

I was dealing with the Oromoni threats which I now posted after 2 years. I was reading what this girl was writing on WhatsApp and vowed never to apologize. LEAVE!! LEAVE!! LEAVE!! Ignore your dáft fans saying it’s not your video.

You wrote the concept. You paid $70k, even the video director needs protection. They are not even “begging on your behalf, the Nigerian way”. If these people harm you, these fans will be the first to post”

Posted on Leave a comment

Marioo kumpa Quick Rocker Million 3

The Hit Man, Toto Bad Omari Ally Mwanga maarufu kama Marioo amesema Yuko Tayari Kumpa Switcher Baba, Quick Rocker bunda kiasi cha TShs. Millioni 3.

Akiwa Gym amekutana na QR na kwa tambo kuhusu wimbo wake ambao amepanga kuutoa Alhamis hii, Marioo amemuahidi Quick Rocker kwamba wimbo wake huo Mpya usipokuwa Hit basi atampa Jamaa Kibunda hiyo.

QUICK ROCKER.

UNAHISI QUICK RACKER ATAKULA HIYO HELA? DONDOSHA COMMENT HAPA CHINI

Posted on Leave a comment

Moto wa Messi, Ageuka Lulu Marekani

Mwanasoka Nguli na kiboko kabisa kutoka Nchini Argentina, Lionel Messi amegeuka Lulu Nchini Marekani.

Ukiachana na Kibunda ndefu aliyovuta kutoka kwenye Club yake Mpya Inter-Miami, Messi amegeuka Kivutio kikubwa sana kwenye soccer la Marekani ambapo Club hiyo imeongeza Idadi Kubwa sana ya Mashabiki Haswa Mastaa Wakubwa wa Marekani kiasi kwamba Tunashuhudia Mastaa wengi wakihudhuria mechi za Club hiyo huku wakionyesha mapenzi yao wazi wazi kwa Nyota huyo.

Kwenye Game yao dhidi ya Atlanta United iliyopigwa tarehe jana, Messi ambaye alichezea Club yake hiyo Mpya kwa mara ya kwanza, alifunga magoli Mawili ya kwanza huku aki assist goli la 3 ambapo Club yake ya Inter-Miami ilipata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Atlanta United.

CHECK HAPA CHINI UNYAMA WA MESSI

Baada ya Game Messi alishow Love kwa Mu-Argentina mwenzake Thiago Almada, ambaye anakipiga Atlanta United.