Posted on Leave a comment

Messi kama sio Genius tu, Basi ni Jini

MESSI

Kama wewe ni mmoja wa waliokuwa wanaamini Messi ndo basi tena zinanywea nyuma, Basi fikiria tena hizo fikra zako.

Pamoja na kwamba ameenda Marekani kuiiinua Ligi kuu ya Mpira wa Miguu kwa Dau kubwa ambalo wengi waliamini kule ndipo Soccer lake linaenda kuzama jua, Messi ameendelea kufanya maajabu kama kawaida yake.

Ukiacha magoli anayoyapiga na kuipaisha Club yake ya Inter Miami, Messi ameendelea pia kupiga magoli yasiyo ya kawaida (Yakufikirika.

Kwenye game yao dhidi ya Club ya Philadelphia usiku wa kuamkia leo ambapo Mchezo huo uliisha kwa Inter Miami kushida Magoli 4-1, Goli la Messi lilikuwa ni goli la ajabu ambapo alifunga akiwa umbali wa Miguu 30 mbali ya Lango la Philadelphia

CHUNGULIA UNYAMA HUO WA MESSI HAPA CHINI:-

Posted on Leave a comment

Moto wa Messi, Ageuka Lulu Marekani

Mwanasoka Nguli na kiboko kabisa kutoka Nchini Argentina, Lionel Messi amegeuka Lulu Nchini Marekani.

Ukiachana na Kibunda ndefu aliyovuta kutoka kwenye Club yake Mpya Inter-Miami, Messi amegeuka Kivutio kikubwa sana kwenye soccer la Marekani ambapo Club hiyo imeongeza Idadi Kubwa sana ya Mashabiki Haswa Mastaa Wakubwa wa Marekani kiasi kwamba Tunashuhudia Mastaa wengi wakihudhuria mechi za Club hiyo huku wakionyesha mapenzi yao wazi wazi kwa Nyota huyo.

Kwenye Game yao dhidi ya Atlanta United iliyopigwa tarehe jana, Messi ambaye alichezea Club yake hiyo Mpya kwa mara ya kwanza, alifunga magoli Mawili ya kwanza huku aki assist goli la 3 ambapo Club yake ya Inter-Miami ilipata ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Atlanta United.

CHECK HAPA CHINI UNYAMA WA MESSI

Baada ya Game Messi alishow Love kwa Mu-Argentina mwenzake Thiago Almada, ambaye anakipiga Atlanta United.

Posted on Leave a comment

Man U waweka Dau kwa Club inayomtaka Maguire

Manchester United wameweka thamani inayotakiwa ya £50m kwa klabu inayotaka kumnunua beki wa England Harry Maguire, 30. (Manchester Evening News)

West Ham wanatumai kumnunua kiungo wa kati wa England James Ward-Prowse, 28, kwa ada ya £20m lakini Southampton wanataka karibu £40m kwa ajili ya nahodha wao huyo (Mail)

Wolves wanakaribia kumsajili tena beki wa pembeni wa Jamhuri ya Ireland Matt Doherty, 31, baada ya kuondoka Atletico Madrid. (TeamTalk)

Uhamisho wa kipa wa Cameroon Andre Onana wa pauni milioni 43 kutoka Inter Milan kwenda Manchester United uko katika hatua za mwisho na utakamilika wiki hii baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kukubaliana maslahi binafsi.

Source: BBC

Posted on Leave a comment

Mo Dewji kuibwaga Simba ‘Nakata Tamaa”

Wakati Mashabiki wa Club ya Simba wakiwa na Shauku kubwa kuona ni kwa namna gani Club hiyo imejipanga katika Msimu ujao, Rais wa heshima wa Club ya Simba na Mfanyabiashara Mohammed Dewji amesema anakaribia kukata tamaa kutokana na mchakato wa mabadiliko wa Club hiyo kutokukamilika hadi sasa ikiwa ni miaka sita sasa tangu awe Mwekezaji katika Club hiyo.

Mapema leo kupitia ukurasa wake wa Twitter Mo ameandika Ujumbe Huu hapa chini:-

NINI MAONI YAKO? TUANDIKIE HAPA CHINI KWENYE COMMENT