Tanasha arudi alipoanzia

Kama ni mtu unayefuatilia, Industry ya Burudani ilianza kumjua Staa wa Kenya Tanasha Donna kupitia Uigizaji wa kwenye Video za Muziki (Video Vixen)

Video ya kwanza ambayo Alionekana ilikuwa Nagharamia, Wimbo wa Ali Kiba na Christian Bella iliyotoka Miaka 7 Iliyopita.

Baadae akawa Mtangazaji wa Kituo cha Radio ya NRG Nchini Kenya ambapo huko ndiko alikokutana na Baba Mtoto wake “Diamond Platnumz”

Kilichofuata baada ya ustaa kumwagiwa Petrol na Mond, Tanasha akajitupa kwenye Muziki ambapo mpaka Sasa ni mmoja kati ya Wasanii wenye Majina Kenya.

Lakini Pamoja na ukubwa huo, bado Tanasha ukienda na Offer inayoeleweka au akikuelewa Bado yupo tayari kuwa Video Vixen kwenye Video yako na ndiyo maana amehusika kama Video Vixen kwenye Video Mpya ya Msanii wa Nigeria Lojay inayokwenda kwa jina la OVA iliyotoka siku 4 zilizopita

CHUNGULIA CHUPA HILO HAPA CHINI KISHA TUPE COMMENT YAKO

UP